Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wazee huteswa na ndugu kisirisiri: Ban

Wazee huteswa na ndugu kisirisiri: Ban

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya uelewa kuhusu ukatili dhidi ya wazee, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni ukweli unaoumiza kwamba mara nyingi wazee hufanywa vitendo vya ukatili na hutelekezwa.

Wakati huu ambapo idadi ya wazee duniani inaongezeka hadi kutarajiwa kufikia asilimia 20 ya raia duniani ifikapo mwaka 2050, ni muhimu kuchukua hatua kwa dharura ili kulinda haki za watu hao, ameongeza Bwana Ban kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo.

Aidha amesema ukatili huu hautekelezwi tu na wale wanaohudumia wazee bali pia ndugu ambao huwatesa wazee kisaikolojia, kifedha na kimwili, na wanawake ndio hatarini zaidi kukumbwa na shida hiyo.

Bwana Ban ameeleza kwa kuwa vitendo hivyo hutokea kisirisiri ndani ya nyumba, ni muhimu zaidi kumulika swala hilo, kulizungumzia wazi na kulipatia jibu la kijamii.