Skip to main content

Punguzo la mgawo wa chakula kwa wakimbizi nchini Kenya laanza: WFP

Punguzo la mgawo wa chakula kwa wakimbizi nchini Kenya laanza: WFP

Punguzo la asilimia 30 la mgawo wa chakula kwa wakimbizi nchini Kenya limeanza leo Jumatatu kufuatia upungufu wa ufadhili na uhaba, limesema Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP.

Katika mahojiano na idhaa hii kutoka Kenya afisa wa mawasiliano wa WFP nchini humo Martin Karim amesema punguzo hilo la mgawo wa chakula litaathiri wakimbizi katika kambi za Daadab na Kakuma ambao wengi wao ni Wasomali na kusisitiza kuwa zoezi hili halitadumu kwa muda mrefu.

(SAUTI MARTIN)

Kwa mujibu wa WFP huenda mgao huo utaendelea hadi Septemba. Imetoa wito kwa jamii ya kimataifa ichangie pengo la ufadhili la dola milioni 40 zinazohitajika hadi Januari mwakani.