Skip to main content

Nchi zinadharau uamuzi wa ICC: Kamishna Zeid

Nchi zinadharau uamuzi wa ICC: Kamishna Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameeleza masikitko yake kwa kitendo cha nchi wanachama wa mkataba wa Roma kupuuza agizo la mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC la kumkamata Rais Omar Al Bashir wa Sudan.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kikao cha 29 cha Baraza la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi akisema nchi wanachama wa mkataba wa Roma zinadharau wazi..

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kikao cha 29 cha Baraza la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi akisema nchi wanachama wa mkataba wa Roma zinadharau wazi..

“Ni kwa mantiki hiyo tunasubiri uamuzi wa mahakama Kuu ya Pretoria asubuhi hii wakati inatathmini ombi lililowasilishwa na ICC”

Halikadhalika amesema miaka sabini baada ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, jamii ya kimataifa inapaswa kuridhika na kuwepo kwa mikataba na sheria mbali mbali zinazolenga kulinda haki za binadamu, akisema bado watu wengi mno wanaishi kwenye mizozo na wanakosa haki zao za msingi.

Amesema huo si wajibu wa viongozi wa dunia pekee, bali pia ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, akitolea mfano wa ripoti za ubakaji nchini Jamhuri ya Afrika ya kati.

Aidha Kamishna Zeid amezungumzia suala la uhamiaji haramu akisema ghasia na mizozo vinasababisha mamilioni kuweka maisha yao hatarini wakijaribu kutafuta hifadhi:

Uhamiaji ni dalili, sababu yake ni kukataa tamaa, baada ya ukiukaji wa mara kwa mara wa haki za binadamu kuondoa matumaini yote ya haki na utu.”