Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani uvamizi wa ubalozi wa Tunisia Tripoli

UM walaani uvamizi wa ubalozi wa Tunisia Tripoli

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya na Mkuu wa ujumbe wa Umoja huo nchini humo, UNSMIL, Bernardino Leon, amelaani vikali uvamizi wa ubalozi wa Tunisia katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, ambao ulitekelezwa na watu wenye silaha, ambao waliwateka nyara wafanyakazi 10.

Ametoa wito wafanyakzi hao wa ubalozi waachiliwe mara moja, na bila masharti yoyote.

Amekumbusha kuhusu kanuni ya kimataifa ya kuheshimu majengo ya kidiplomasia na ubalozi. Ametoa wito kwa wote wenye ushawishi Libya wafanye kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa wanadiplomasia hao wa Tunisia wanaachiliwa salama, na kulinda balozi za kigeni nchini Libya.