Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashauriano kuhusu Yemen kuanza kesho Juni 15

Mashauriano kuhusu Yemen kuanza kesho Juni 15

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, ametangaza leo kuanza kwa mashauriano ya awali jumuishi kuhusu Yemen kuanzia kesho, Juni 15, 2015, chini ya Umoja wa Mataifa.

Mashauriano hayo ya awali yanatarajiwa kuwaleta pamoja pande za kisiasa za Yemeni, zikiwemo GPC, Ansar Allah, JMP na Hirak.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa wawakilishi wa kisiasa wa Yemen washiriki katika mashauriano hayo kwa wema na bila masharti, na katika mazingira ya kuaminiana na kuheshimiana, ili waweze kupata njia za kuanzisha tena mchakato wa kisiasa na kufikia suluhu litakaloikoa Yemen na watu wake kutokana na mzozo uliopo sasa.