Ulemavu wa ngozi si kikwazo kwangu: Mbunge Mwaura

Ulemavu wa ngozi si kikwazo kwangu: Mbunge Mwaura

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha tarehe 18 disemba mwaka 2014 lilipitisha azimio namba 69/170 la kuanzisha siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu ulemavu wa ngozi. Uamuzi huo ulizingatia madhila wanayokumbana nayo kundi hilo kiuchumi, kisiasa na kijamii.Mathalani kukatwa viungo vyao kwa imani za kishirikina, kunyimwa haki za msingi kama vile elimu, afya na hata kutengwa. Azimio linataka pamoja na mambo mengine serikali kuchukua hatua kubadili mtazamo hasi wa jamii dhidi ya kundi hili na kuhakikisha wanaishi maisha sawia na binadamu wengine. Hali barani Afrika ikoje?