Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenye nyumba wanaogopa hata kutupangisha kisa ngozi yetu: Al Shaymaa

Wenye nyumba wanaogopa hata kutupangisha kisa ngozi yetu: Al Shaymaa

Hatimaye dunia inaanza kuadhimisha siku ya kuhamasisha jamii kuhusu ulemavu wa ngozi, au Albinism. Ukosefu wa uelewa juu ya hali hiyo ya kiafya imesababisha kundi hilo kukumbwa na madhila kila uchao, ikiwemo baadhi kukatwa viungo vyao eti vinaleta utajiri. Nchini Tanzania mauaji ya Albino yalishika kasi hadi Umoja wa Mataifa ukataka serikali ichukue hatua.

Na kama hiyo haitoshi sasa, kuna siku  maalum ambayo ni Juni 13 ya jamii kuelimishana kuwa ni hali ya kawaida na wana haki sawa na binadamu wengine na wapatiwe haki za msingi za kibinadamu ili washamiri katika maisha yao.

Mbunge Al Shaymaa Kwegyir kutoka Tanzania ambaye pia ni mlemavu wa ngozi, amehojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ambapo pamoja na kuelezea maisha ya utotoni yalikuwaje, anaanza kusema vile amepokea uwepo wa siku hii..