UNRWA yaanza mpango wa elimu wa majira ya joto

12 Juni 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limeanza mpango wake wa  mafunzo katika kipindi cha majira ya joto SLP ambao utawapa fursa  watoto walioanguka masomo ya Kiarabu na Hisabati au yote mawili kusawazisha alama zao na kuendelea katika daraja la juu.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNRWA wanafunzi walioanguka masomo hayo wamefahamishwa kuhudhuria SLP ambapo watahudhuria masomo maalum yaliyoandaliwa na wataalamu wa elimu kutoka  shirika hilo.

UNRWA inasema kuwa wanafunzi watahudhuria darasani kwa siku 18 kuanzia Juni nane na kufanya mtihani wa mwisho wa kiarabu June 29 na wa Hisabati mnamo June 30.

Mkuu wa mpango wa elimu katika shirika hilo Farid Abu Athra anasema anajivunia mpango huo ambao huwapa fursa ya pili na muhimu wanafunzi kutokana na kile ambacho walikikosa kwani wengi wao wanakumbana na madhila ya machafuko katiak ukanda wa Gaza.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter