Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umekaribisha mchango wa dola milioni 300 kutoka Kuwait

UM umekaribisha mchango wa dola milioni 300 kutoka Kuwait

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, imekaribisha tamko la mchango wa dola milioni 200 kutoka Kuwait kwa ajili ya kusaidia watu walio na mahitaji Iraq huku ikitangaza pia mchango wake wa dola milioni 100 kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Yemen.

Rashid Khalikov, Murugenzi wa OCHA mjini Geneva Uswisi, amesema ufadhili kutoka Kuwait kwa ajili ya kusaidia watu walio na mahitaji Iraq na Yemen ni ishara ya jukumu ambalo Kuwait imechukua katika juhudi zake za usaidizi wa misaada ya kibinadamu kote ulimwenguni.