Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria nchini Kenya yaleta unafuu kwa ustawi wa watu wenye ulemavu

Sheria nchini Kenya yaleta unafuu kwa ustawi wa watu wenye ulemavu

Wakati mkutano wa Nane wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa kuhusu haki za watu wenye  ulemavu ukiendelea jijini New York, serikali ya Kenya imetaja hatua ambazo imechukua kuimarisha ustawi wa kundi hilo ikiwa ni kwa mujibu wa sheria ya watu wenye ulemavu.Kiongozi wa ujumbe wa Kenya kwenye Lydia Muriuki ametaja hatua hizo alipozungumza na Idhaa hii.

(Sauti ya Lydia)

Naye Mwenyekiti wa Baraza la watu wenye ulemavu nchini Kenya Dkt. David Ole Sankok ambaye naye anaishi na changamoto ya ulemavu, amesema maisha ya kundi hilo yanaanza kutiwa nuru akisema usaidizi huo umeenda hadi kwenye elimu kwa kuwa kila mwezi..

(Sauti ya Dkt. David)

Sanjari na kuboresha hifadhi ya jamii kwa kupatiwa fedha na msaada wa elimu, ibara ya 54 ya Katiba ya Kenya inatenga asilimia Tano ya uteuzi wa fursa za ajira iwe ni watu wenye ulemavu, sanjari na asilimia mbili ya manunuzi yote ya serikali inapaswa ifanywe na watu wenye ulemavu.