Skip to main content

Boko Haram na madhila kwa wananchi huko Afrika Magharibi

Boko Haram na madhila kwa wananchi huko Afrika Magharibi

Ghasia zinazofanywa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram huko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na nchi jirani kama vile Cameroon na Chad zimesababisha mamia ya maelfu ya wakimbizi wa ndani nan je. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takribani watu Laki Mbili wamesaka hifadhi Cameroon, Niger na Chad kutokana na kukimbia makazi yao huko Nigeria. Na wakati mwingine Boko Haram hushambulia hata maeneo yanayohifadhi wakimbizi hao hali inayosababisha sintofahamu kwa wananchi, hususan wanawake na watoto. Je hali ikoje? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.