Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eritrea na Ethiopia miongoni mwa nchi zilizomulikwa kuhusu Haki za mtoto

Eritrea na Ethiopia miongoni mwa nchi zilizomulikwa kuhusu Haki za mtoto

Kamati kuhusu haki ya mtoto, imekamilisha tathmini yake ya hali ya haki za mtoto katika nchi kadhaa wanachama, ikitoa picha yenye mseto wa mambo kuhusu hatma ya watoto katika nchi hizo.

Huyu hapa ni Benyam Mezmur, mwenyekiti wa kamati hiyo, akikutana na waandishi wa habari mjini Geneva

“Hii inahusu nchi tulizofanyia tathmini katika kikao chetu cha 69, kati ya Mei 18 na Juni 5, katika muktadha wa Mkataba kuhusu Haki za Mtoto, na ni Eritrea, Ethiopia, Ghana, Honduras, Mexico na Uholanzi.

Wanakamati hiyo wamesema, nchini Mexico kuna ripoti za mauaji ya wanawake na wasichana kwa viwango vya juu mno, pamoja na kutoweka kwa watoto, hususan wasichana kuanzia umri wa miaka kumi.

Nchini Eritrea, kamati hiyo imesema watoto wa kike wanabaguliwa, huku kukiwa na viwango vya juu vya ndoa na mimba za utotoni.