Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yarejesha shuleni watoto 400,000 Sudan Kusini

UNICEF yarejesha shuleni watoto 400,000 Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini, ni asilimia 42 tu ya watoto wanaenda shuleni, hii ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, huku asilimia 70 ya shule zilizopo kwenye maeneo ya mapigano zikiwa zimefungwa kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoibuka nchini humo mwezi Disemba mwaka 2013.

Kuanzia mwezi Februari mwaka huu, UNICEF imeanzisha mradi wa kuwarejesha shuleni watoto 400,000 ambao hawakuwahi kwenda shuleni au wameacha shule, wakiwa ni watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitatu hadi 18.

Jimbo la Equatoria Maghiribi ni moja ya maeneo ambapo mradi huu umeanzishwa hivi karibuni ikiwa ni hatua ya mwisho baada ya kampeni kuzinduliwa katika majimbo mengine hapo awali. Kulikoni ? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.