WFP na mafanikio kwa wakulima Uganda
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchin Uganda linajivunia mafanikio kutokana na miradi yake ya kuongeza uzalishaji na ubora wa nafaka miongoni mwa wakulima wadogo nchini humo ambako sasa wanaweza kuuza nafaka yao kwenye masoko ya kimataifa.Taarifa kamili na John Kibego.
(Taarifa ya John Kibego)
Kaimu Mwakilishi wa WFP Uganda, Michael Danford amesema, kutokana na uwekezaji wao wa dola Milioni 32 milioni tangu mwaka 2009, wamefanikiwa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kwa tani 25,000.
Amesema shirika hilo limetoa taarifa muhimu, kuwapa ujuzi na kutoa vifaa vya kisasa kwa zaidi ya vikundi 1,000 vya wakulima.
Bwana Dunford amehusisha mafanikio yote na ujenzi na ukatabati wa maghala makubwa tisa na vifaa 46 vya kijamii vya kuhifadhi nafaka katika wilaya za Gulu, Jinja, Soroti, Kasese, Kapchorwa, Lira and Masindi.
Katika miaka sita iliyopita, WFP limenunua zaidi ya tani 41,000 za chakula kutoka wakulima wadogo na wafanyabiashara baada ya wingi na ubora wa idhaa zao kuimarishwa.