Mlipuko wa Kipindupindu Kigoma , Tanzania umekuwa fundisho: Mtaalamu

9 Juni 2015

Ikiwa tayari jitihada za serikali ya Tanzania na wadau wa afya zimewezesha kudhibiti mlipuko wa Kipindupindu miongoni mwa wakimbizi wa Burundi na wananchi huko Kigoma nchini humo, mmoja wa wataalamu wa afya walioshiriki jitihada hizo ametaja kile kilichofanikisha udhibiti wa haraka wa ugonjwa huo.

Jacob Lusekelo ambaye ni mwanasayansi wa maabara kutoka Maabara kuu ya Taifa nchini humo ameiambia Idhaa hii kuwa hatua ya shirika la afya ulimwenguni, WHO kusaidia kuongeza nguvu ya watendaji ni moja ya siri.

(Sauti ya Lusekelo)

Akasema hiyo ilikuwa ni fundisho na sasa hatua zimechukuliwa kudhibiti iwapo mlipuko unatokea tena

(Sauti Lusekelo)

Ugonjwa wa Kipindupindu ulilipuka mkoani Kigoma na kusababisha vifo vya watu 30 baada ya mmiminiko wa wakimbizi kutoka Burundi kuingia nchini Tanzania kufuatia ghasia nchini mwao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter