Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo kuhusu Libya yaanza tena huko Morocco, Ban afuatilia kwa karibu

Mazungumzo kuhusu Libya yaanza tena huko Morocco, Ban afuatilia kwa karibu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anafuatilia kwa karibu mashauriano kuhusu Libya yaliyoanza tena hii leo huko Morocco.

Hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alipozungumza na waandishi wa habari akisema kuwa yanafuatia mikutano ya wawakilishi wa manispaa na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika Tunisia na Algeria wiki iliyopita.

Habari zinasema kuwa mwakilishi maalum wa Katibu mkuu huko Libya, Bernardino León, atawasilisha rasimu mpya ya makubaliano kwa wawakilishi hao wa vikundi kutoka Libya.

Umoja wa Mataifa unashukuru kitendo cha mataifa mengi ikiwemo nchi wanachama wake nan chi jirani kuunga mkono mazungumzo hayo, ukisema kuwa unatarajia mkutano huo utafanikisha kupatikana kwa makubaliano ya kuanzishwa kwa serikali ya maridhiano ya kitaifa.