Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu akariri uungaji wake mkono kwa Mjumbe wake kwa maziwa makuu

Katibu Mkuu akariri uungaji wake mkono kwa Mjumbe wake kwa maziwa makuu

Kufuatia barua zilizotumwa na vyama mbalimbali vya upinzani nchini Burundi vikiomba Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kwa Maziwa Makuu Said Djinnit ajiuzulu, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema Katibu Mkuu anakariri uungaji wake mkono kwa Mjumbe huyo.Akijibu swali la mwaandishi wa habari leo mjini New York, Bwana Dujarric amesema Katibu Mkuu anamwamini Mjumbe huyo maalum ambaye amepewa jukumu la kuratibu mazungumzo ya amani nchini Burundi. Aidha amesema Ban Ki-moon anampongeza Bwana Djinnit kwa jitihada zake katika kushirikisha pande zote pamoja na viongozi wa ukanda mzima.

Halikadhalika Bwan Dujarric amesema Katibu Mkuu anaamini kuwa ni lazima pande zote za mzozo wa Burundi zifikie makubaliano mara moja ili kuandaa uchaguzi jumuishi wenye usawa na uhuru, akizisihi kuweka maswala ya amani na maridhiano mbele ya manufaa yao ya kisiasa.