Maelfu ya wapalestina hatarini kuhamishwa na Israel, mtaalam wa UM aonya

5 Juni 2015

Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye maeneo ya Palestina yaliyokaliwa tangu 1967, Makarim Wibisono, leo amekariri wito wake kwa serikali ya Israel kusitisha mpango wake wa kuhamishia wapalestina mabedui kwenda katikati ya ukingo wa magharibi.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Haki za Binadamu, mtaalam huyo amesema uhamisho huo, ambao utekelezaji wake unakaribia, utalazimisha maelfu ya watu kuhama makwao ukiwa kinyume na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

Amesikitishwa kwamba wito wake wa awali wa Oktoba, 2014, haukusikilizwa na serikali ya Israel.

Bwana Wibisono ameongeza kuwa takriban theluthi mbili ya watu wanaotarajiwa kuhamishwa ni watoto.

Tangu kuteuliwa kwake mwezi Juni mwaka 2014, mtaalam huyo hajaruhusiwa kusafiri Israel wala kwenye maeneo yaliyokaliwa ya Palestina.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter