Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNEP na Yaya Toure washabikia gari rafiki kwa mazingira

Mkuu wa UNEP na Yaya Toure washabikia gari rafiki kwa mazingira

Msaidizi wa Katibu Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Achim Steiner pamoja na mchezaji maarufu wa mpira wa miguuambaye pia ni Balozi Mwema wa UNEP Yaya Touré wameingia pamoja kwenye maonyesho ya Milan, Italia, Expo Milan 2015 kwa kutumia gari lililobadilishwa injini na kuendeshwa na umeme.

Tukio hilo lilifanyika leo wakati ambapo Umoja wa MAtaifa unaadhimisha siku ya kimataifa ya mazingira kote duniani.

Injini ya gari hilo aina ya Fiat imebadilishwa na badala yake kuwekwa injini ya umeme na betri kwa kampuni ya kiitaliano Confartigianato, UNEP ikisema ni mfano wa kuonyesha jinsi gani vifaa vya zamani vinaweza kuhuishwa na kutumiwa upya na teknolojia rafiki kwa mazingira.

Kwa mujibu wa UNEP, uchafuzi utokanao na vyombo vya usafiri ni asilimia 80 ya uchafuzi wa hewa mijini, UNEP ikiongeza kwamba magari yanayotumia nishati mbadala yanaweza kuimarisha afya ya wakazi wa miji.

Katika video iliyotolewa leo na UNEP, Yaya Touré ameshangilia gari hilo akisema:

(SAUTI YAYA)

“ Kwangu kama balozi mwema ni lazima kuanza na kitu kimoja. Kwa sababu wachezaji wengi, kama mimi au wenye umri mdogo kuliko wangu wanapenda magari makubwa, POrshe, Ferrari, ambayo hayaendeshwi na umeme. Kwa hiyo itakuwa mfano mzuri mikijaribu moja ya magari hayo ” .