Skip to main content

Kunyamazisha waandishi habari kunadhoofisha haki za binadamu Iran:Mtaalam UM

Kunyamazisha waandishi habari kunadhoofisha haki za binadamu Iran:Mtaalam UM

Kushikiliwa kwa waandishi wa habari na watetezi wa haki za bindamu kunadhoofisha ulinzi wa haki za binadamu kwa watu wa Iran, hii ni kulingana na Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa Ahmed Shaheed Ijumaa. Bwana Shaheed ameelezea kusikitishwa kwake na ukamataji wa kiholela, kuzuiliwa na kushtakiwa kwa waandishi habari na wanaharakati nchini humo.

Mtaalamu huyo ambaye ameteuliwa na Baraza la Usalama la haki la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini Iran amesema kwamba kunyamazisha sauti hizi kunaathiri mazungumzo ya umma na kuwanyima watu wa Iran na ulimwengu mzima kwa ujumla taarifa muhimu kuhusu hali nchini humo.

Kadhalika amesema kwamba madai ya kuhatarisha usalama wa taifa, propaganda dhidi ya mamlaka na matusi kwa ajili ya kushtaki na kuwazuilia wanahabari na wanaharakati ni kinyume na haki za kujieleza na kujumuika na ni ukikwaji wa sheria.

Bwana Shaheed ameelezea kusikitishwa na kukamatwa na kuzuiliwa na kushtakiwa kwa Jason Rezaiana ambaye mwandishi wa habari kutoka Washington Post na mkewe Yeganeh Saleh, ambaye anafanya na gazeti la kitaifa la UAE The National.