Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo endelevu bila kuharibu mazingira: Ban

Maendeleo endelevu bila kuharibu mazingira: Ban

Ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema lengo la maendeleo endelevu ni kukuza kiwango bora cha maisha kwa wote bila kuongeza uharibu wa mazingira na rasilimali ambazo ni mahitaji kwa mustakabli wa kikazi kijacho.

Katika ujumbe wake kwa njia ya video ambao umesheni pia wadau mbalimabli wa mazingira Bwana Ban amesema hilo linawezekana kwa kubadili mfumo wa matumizi ya bidhaa kwa kutumia zile ambazo hutumia nishati  maji na rasilimali nyingine kwa kiwango kidogo.

(SAUTI BAN)

Akiongea kuhusu utunzanji wa mazingira mkurugenzi wa mazingira katika ofisi ya Makamu wa Rasi wa Tanzania Julius Ningu amesema kile ambacho ni muhimu katika maadhimisho haya.

(SAUTI NINGU)

Siu ya mazingira duniani kimataifa itaadhimishwa nchini Italia nchi ambayo ni mafano katika utunzanji  wa mazingira.