Niger yaridhia mkataba wa kutokomeza utumwa wa kisasa

5 Juni 2015

Niger imekuwa nchi ya kwanza kuridhia marekebisho ya mwaka 2014 ya mkataba wa Shirika la Ajira Duniani, ILO kuhusu ajira za kulazimishwa, kama sehemu ya juhudi mpya za kimataifa za kutokomeza ajira za lazima, ukiwemo usafirishaji haramu wa watu na vitendo vya utumwa wa kisasa.Taarifa ya Joshua Mmali inafafanua zaidi.(Taarifa ya Joshua)

Akizungumza kufuatia hafla ya uridhiaji huo wa Niger, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Guy Ryder amesema anatumai nchi zaidi zitauridhia ili uanze kuutekelezwa, akiongeza kuwa hatua ya Niger inawapa matumaini mamilioni ya wanawake, watoto na wanaume ambao wamenaswa katika utumwa wa kisasa.

ILO inakadiria kuwa kote duniani, watu milioni 21 ni waathirika wa ajira za lazima, wengi wao wakinyanyaswa katika kilimo, uvuvi, ajira za nyumbani, ujenzi, usindikaji, uchimbaji migodi na nyinginezo.

Imeongeza kuwa wanawake na wasichana hasa hukumbwa na unyanyasaji wa biashara ya ngono.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter