Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkandarasi aliyekiuka kanuni za usafirishaji huko Darfur kufutwa kwenye orodha:UNAMID

Mkandarasi aliyekiuka kanuni za usafirishaji huko Darfur kufutwa kwenye orodha:UNAMID

Huko Darfur nchini Sudan watu wasiojulikana majuzi walishambulia msafara uliokuwa na magari ya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika nchni humo, UNAMID. Magari manne kati ya matatu yalitekwa nyara na kuibua sintofahamu ya usalama wa usafirishaji wa vifaa hivyo adhimu wakati huu ambapo katika eneo hilo hali ya kuzorota kwa usalama imekuwa ikiripotiwa. Je nini kilitokea na hatua gani zimechukuliwa? Assumpta Massoi wa idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu kutoka El Fasher na Kamanda Mkuu wa vikosi vya UNAMID, Luteni Jenerali Paul Mella ambaye anaanza kwa kuelezea kilichojiri.