Kampeni dhidi ya Fistula yapamba moto Tanzania: UNFPA

Kampeni dhidi ya Fistula yapamba moto Tanzania: UNFPA

Kampeni inayoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA ya kuhamasisha kuhusu athari na matibabu ya ugonjwa wa Fistula unaowapata wanawake baada ya kujifungua inaendela nchini Tanzania ambapo timu maalum ikiwahusisha wasanii wa muziki wanazunguka mikoa mbalimbali kuelimisha umma.

Katika mahojiano na idhaa hii msaidizi wa mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini Tanzania Dkt. Rutasha Dadi anaeleza matokeo ya kampeni hiyo hadi sasa.

(SAUTI DK RUTASHA)

Kampeni hiyo inatarajiwa kuhitimishwa jumamosi juma hili.