Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atangaza kupitiwa upya kwa uchunguzi wa tuhuma za ukatili wa kingono CAR

Ban atangaza kupitiwa upya kwa uchunguzi wa tuhuma za ukatili wa kingono CAR

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon ametangaza kufanyika kwa mapitio ya namna mifumo ya Umoja wa Mataifa ilivyoshughulikia tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Akiongea na waandishi wa habari mjiniNew York msemaji wa Katibu Mkuu Stephanie Dujarric amesema kazi hiyo itafanywa kundi la nje na huru lisilofungana na upande wowote na kwamba ,

(SAUTI DUJARRIC)

‘‘Mapitio yatachunguza namna ripoti ya ukatili huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ilivyoshughulikiwa na ukubwa wa masuala yanayohusiana na namna Umoja wa Mataifa unavyomaanisha katika kushughulika taarifa za jinsi hii.’

Bwana Dujarric amesema kuwa kama ilivyoelezwa katika majuma ya hivi karibuni Katibu Mkuu anahuzunishwa kwa kina na tuhuma za ukatili wa kijinsia CAR na namna pande mbalimbali za Umoja wa Mataifa zilivyoshugulikia tuhuma hizo.

Amesema lengo la kutangazwa kwa mpango huo ni kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa hautelekezi waathiriwa wa ukatili wa kijinsia hususani pale ukatili huo unaopotendwa na wale wanaopaswa kuwalinda.

Kwa mujibu wa Dujarric, katika siku chache zijazo watatangaza majina ya wanaoongoza mapitio na hadidu za rejea.