Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Boko Haram wafanya ukatili kwa raia Cameroon: UM

Boko Haram wafanya ukatili kwa raia Cameroon: UM

Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu nchini Cameroon Najat Rochdi ameonya kuwa waasi wa kundi la kigaidi la Boko Harama waliotapakaa wanafanya vitendo vya kigaidi kwa raia wa Cameroon walio katikamazingira magumu huku wakijikusanya upya kwa ajili ya mashambulizi. Taarifa zaidi na Amina Hassan .

(TAARIFA YA AMINA HASSAN)

Mratibu huyo wa masuala ya kibinadamu amesema kuwa waasi hao kutoka Nigeria wanavuka mpaka kuingia Cameroon ambapo wanatenda vitendo vya kinyama ikiwamo kuteka nyara watoto, na kuchoma mazao kaskazini mwa nchi.

Amesema kuwa ukatili huo unaofanya na Boko Haram unaendelea akati ambapo wakimbizi wa 100,000 nchini Nigeria wanakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Bi Rochdi amesema vitendo hivyo vinakwamisha ustawi wa jamii kwani huduma muhimu mathalani za matibabu zinadorora kwa kuwa.

(SAUTI ROCHDI)

Wanateka watoto nyara na kuwatumikisha jeshini au kama “silaha ndogo” jinsi wanavyowaita. Pili, wanaharibu kabisa uchumi, wanazuia usafiri wa jamii, na kwa hiyo masoko kule yamefungwa kabisa kwa sababu hakuna kitu cha kuuza.”