Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitandao ya kijamii na mwelekeo wa ugaidi: Feltman

Mitandao ya kijamii na mwelekeo wa ugaidi: Feltman

Mkutano kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika kukabiliana na ugaidi umefanyika hii leo hapa makao makuu ambapo wadau wa mapambano hayo kutoka tasinia ya habari na sekta nyingine wameeleza namna vyombo hivyo vinavyoweza kutumika kama silaha ya kutokomeza ugaidi.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maswala ya kisiasa, Jeffrey Feltman amesema mitandao ya kijamii ina nguvu lakini sasa inaonekana ni tishio kubwa katika kuchochea ugaidi.

(SAUTI FELTMAN)

“Ujumbe wa hila unaochochea misimamo mikali ambayo hutumwa kupitia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Youtube na mingineyo inavutia na kuhadaa vijana wanaosaka mambo mbadala ya ajabu. Kuna takribani akaunti Elfu 50 zinazounga mkono magaidi wa ISIS. Serikali zinajitahidi kutuma ujumbe zaidi wa kubadili ujumbe huo wa chuki. Vijana hawasaki mambo ya msimamo wa kati, wanasaka kile kinacholenga dira zao na kugusa fikra zao na kuleta mabadiliko ya dhati.”

Amesema zaidi ya watu 25,000 wamesafiri kueleka Syria na Iraq kujiunga na vikundi vya kigaidi msukumo mkubwa ukitokana na mitandao hiyo ya kiijamii huku idadi hiyo ikiongezeka.