Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yasikitishwa na msemakweli Myanmar kufungwa jela

OHCHR yasikitishwa na msemakweli Myanmar kufungwa jela

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imesema inasikitishwa na kitendo cha serikali ya Myanmar kumhukumu adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela U Htin Lin Oo kwa kosa la kutusi dini.

Msemaji wa Ofisi hiyo Ravina Shamdasani amesema alichofanya U Htin si kutusi dini bali kuzungumza kitendo cha matumizi ya imani ya kibuda kwa misimamo mikali na hivyo adhabu dhidi yake ni tofauti na wale ambao wanachochea chuki dhidi ya kundi la watu wachache wa jamii ya Rohingya.