Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ya Mashariki yakumbwa na athari za biashara haramu ya tumbaku: WHO

Afrika ya Mashariki yakumbwa na athari za biashara haramu ya tumbaku: WHO

Biashara haramu ya tumbaku inaathiri pia Ukanda wa Afrika Mashariki amesema Mshauri wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu tumbaku barani Afrika, Daktari Ahmed Ogwell Ouma wakati huu ambapo WHO imeadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku kwa kuangazia athari za biashara haramu ya tumbaku, ambazo ni asilimia 10 za sigara zinazouzwa duniani kote.

Akihojiwa na Idhaa hii, Daktari Ouma ameeleza kuwa biashara hizo ni za aina tatu: magendo ya sigara, sigara bandia na sigara zisizo na idhini kabisa, akifafanua athari zake.

(Sauti ya Ouma 1 )

Na akatoa wito kwa watumiaji wa sigara Afrika ya Mashariki.

(Sauti ya Ouma 2 )