Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ili mitandao ya kijamii isigeuke shubiri, tuzingatie kanuni- Mungy

Ili mitandao ya kijamii isigeuke shubiri, tuzingatie kanuni- Mungy

Jukwaa la dunia kuhusu ulimwengu wa mawasiliano lilifunga pazia lake hivi karibuni huko Geneva, Uswisi ambapo wajumbe wa nchi shiriki walipata fursa ya kujifunza mengi ili kuhakikisha maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  yanakuwa na faida badala ya kugeuka shubiri kwa watumiaji. Miongoni mwa washiriki ni Innocent Mungy, Meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA ambaye alimweleza Assumpta Massoi wa idhaa hii katika mahojiano ya njia ya simu kutoka Geneva, kuwa jukwaa lilikuwa kisima cha mafunzo. Lakini vile vile aliangazia sheria ya makosa mtandao iliyopitishwa hivi karibuni nchini Tanzania. Je amesema nini, fuatana nao katika mahojiano haya, akianza kwa kujibu maana ya kuongezeka kwa watumiaji wa intaneti duniani ambao mwishoni mwa mwaka huu itafikia Bilioni 3.2.