Skip to main content

Serikali ya Somalia iendelee kujenga uwezo wake apendekeza mtalaam wa Umoja wa Mataifa

Serikali ya Somalia iendelee kujenga uwezo wake apendekeza mtalaam wa Umoja wa Mataifa

Wakati huu ambapo Somalia inaelekea kuandaa uchaguzi wa rais na wabunge  mwaka 2016 na kuunda katiba mpya, Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu nchini Somalia, Tom Nyanduga, ameeleza changamoto alizozishuhudia wakati wa ziara yake ya pili nchini humo kwanzia tarehe 22 hadi 29 mwezi Mei.

Licha ya jitihada za serikali kwa upande wa usalama na ujenzi wa taifa, Bwana Nyanduga ameeleza wasiwasi wake kuhusu usalama kwenye kambi za wakimbizi wa ndani na uhuru wa vyombo vya habari ambapo katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa Idhaa hii ametoa wito kwa serikali ya Somalia, pamoja na kupambana na kundi la Al-Shabaab, ihakikishe kuwa wanajenga uwezo wa tasisi za nchi hii ili raia waendelee kupata haki zao.

Lakini kwanza anaanza kwa kufafanua mafanikio aliyoyashuhudia.