Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMO yatoa mwongozo wa kunusuru wakimbizi na wahamiaji baharini

IMO yatoa mwongozo wa kunusuru wakimbizi na wahamiaji baharini

Shirika la Kimataifa la Ubaharia limetoa mwongozo mpya kuhusu uokoaji wa wakimbizi na wahamiaji waliokwama baharini.

Mwongozo huo wenye maelezo mapya umechapishwa katika lugha sita, ukitoa pia mwelekeo wa sheria kuhusu njia zinazoweza kuhakikisha kuwa watu walionusuriwa, hususan wakimbizi na wahamiaji, wanawezeshwa kushuka ufukweni, na jinsi ya kukidhi mahitaji yao.

Mwongozo huo umeandaliwa kwa pamoja na IMO, Baraza la Kimataifa la Mabaharia, ICS, na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, na unalenga kutumiwa na manahodha, wamiliki wa meli na serikali.