UNAMA yalaani vifo vya watoa misaada

2 Juni 2015

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umeelezea kusikitishwa kwake na kuuwawa kwa wafanyakazi tisa wanaohudumu katika mashirika ya kutoa misaada kwa wahitaji.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa UM nchini Afghanistan Mark Bowden, amenukuliwa akisema kuwa anashangazwa tena kwa vifo vya wafanyakazi hao ambao wanatoa msaada unaohitajika kwa wingi nchini humo.

Mauji hayo yametokea katika shambulio la usiku katika jingo la shirika la misaada kaskazini mwa nchi jimboni Balkh ambapo hakuna upande ambao umedai kuhusika na mauaji hayo hadi sasa.

Bwana Bowden ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya Afghanistan amesema anaungana na wafanyakazi wenzake katika huzuni kufuatia kuondokewa na wenzao pamoja na familia za marehemu .

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter