Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yaadhimisha miaka 65, yahimiza ulinzi wa haki za wakimbizi

UNRWA yaadhimisha miaka 65, yahimiza ulinzi wa haki za wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo limeadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwake kwa kufanya mkutano maalum unaoangazia uwezeshaji wa maendeleo endelevu na ulinzi wa haki za wakimbizi wa Kipalestina.

Taarifa Zaidi na Joshua Mmali.

(TAARIFA YA MMALI)

(Nats)

Video fupi inayoonyesha safari ya UNRWA kwa miaka 65 ikiionyeshwa katika ukumbi hapa Umoja wa Mataifa kabla ya kuanza kwa hotuba za washiriki wa mkutano huu.

Wakimbizi wawili wa Kipalestina wamehudhuria mkutano huu kuelezea mateso na adha wanazokumbana nazo, akiwemo mama huyu anayeeleza mkasa wake kwa uchungu.

(SAUTI)

"Mimi ni Lina Meri nina mabinti wawili ambao wako chuoni, kama mama mwingine yeyote mabinti hawa ni vipaumbele vyangu. Licha ya kukatishwa tamaa natafuta fursa salama wao kusoma na kuwa na maisha bora." 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema umoja huo utaendelea kutoa usaidizi wa kimaendeleo na ulinzi wa haki za wakiimbizi huku akisikitishwa na madhila wanayokumbana nayo wakimbizi wa Kipalestina walioko katika kambi ya Yarmouk nchini Syria.

(SAUTI)

"Raia huko Yarmouk hawana pa kukimbilia, pande kinzani zina wajibu wa kukomesha machafuko zaidi kambini na kuruhusu misaada iwafikie wahitaji."