Skip to main content

Nchi za Afrika zaweza kunufaika na mabadiliko ya idadi ya watu : UNFPA

Nchi za Afrika zaweza kunufaika na mabadiliko ya idadi ya watu : UNFPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA Babatunde Osotimehin, amesema ongezeko la idadi ya watu nchini Nigeria ambayo sasa raia zaidi ya Milioni 170 ni changamoto kubwa.

Bwana Osotimehin, ambaye aliwahi kuwa waziri wa afya nchini Nigeria amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kutumia mabadiliko ya mwelekeo wa idadi ya watu kuleta mafanikio.

Ameeleza kwamba nchi za bara la Afrika zinaweza kunufaika na mabadiliko hayo ambapo vijana wa siku hizi hawana majukumu mengi ya kulea watoto wengi, na hivyo wanakuwa na fursa ya kujiendeleza zaidi kiuchumi na kuleta maendeleo nchini mwao.

Lakini amesisitiza kwamba serikali za Afrika zinapaswa kuwekeza zaidi katika maendeleo ya vijana ili wanufaike na mabadiliko haya, na kwa hiyo inafaa…

«  kuwezesha serikali kuelewa kwamba mtaji wao ni watu, na wanahitaji kuwekeza katika wao ili kuleta mabadiliko. Natumaini serikali zote zitafanya uwekezaji na kutengenza mazingira yanayohitajika ili kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo. Mataifa yatafaidika, dunia pia. »