Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukandamizi dhidi ya mashoga, wasagaji na wabadili jinsia unaendelea:OHCHR

Ukandamizi dhidi ya mashoga, wasagaji na wabadili jinsia unaendelea:OHCHR

Ofisi  ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imetoa ripoti mpya inayoendelea kudhihirisha ubaguzi na  ukatili dhidi ya mashoga, wasagaji na watu waliobadili jinsi zao.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa ripoti hiyo mpya ni ushahidi wa pili rasmi unaoonyesha kuwa watu wanabaguliwa kwa misingi ya mwelekeo wa jinsi zao ambapo imetoa mapendekezo 20 kwa serikali za kitaifa ikiwemo..

(Sauti ya Farhan)

“Kutambua kisheria mahusiano ya jinsia moja, kuhakikisha kunakuwepo kwa nyaraka za kutambua jinsia ya mtu, na kuondokana na tiba kandamizi zinazolenga kugeuza mwelekeo wa mtu ambao anahisi amekuwa nao licha ya kuzaliwa na jinsia nyingine, kufunga vizazi kwa lazima na mbinu nyingine za matibabu kwa watoto  waliozaliwa na jinsia mbili.”