Skip to main content

Kuzorota kwa usalama kwakwamisha chakula cha msaada kufika Yemen: WFP

Kuzorota kwa usalama kwakwamisha chakula cha msaada kufika Yemen: WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) limesema misaada muhimu ya chakula kilichokuwa kinaelekea Yemen kime kwama katika bandari ya Eden kufuatia taarifa za kuendelea kwa mapigano na tishio la usalama.

Meli ya MV Amsterdam iliyokuwa njiani kutokea Djibouti ikiwa imebeba tani 5700 za chakula ikiwamo ngano, kunde, mboga mboga na chembe chembe za virutubisho kwa ajili ya kulinda watoto dhidhi ya utapiamlo na upungufu wa damu. Chakula hicho kililenga kuwafikia raia 60,000 na kuwatosheleza kwa mahitaji ya mwezi mmoja.

Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP mjini Geneva

«  Licha ya matatizo, tumeweza kuwafikia waYemen milioni moja na nusu tangu mwezi wa Aprili. Tunapaswa kuendelea. Kweli kuna sehemu kusini mwa Yemen ambazo hazifikiki. Lakini tunajitahidi sana ili kutumia uwezekano wowote wa kusambaza misaada ya kibinadamu licha ya mazingira magumu sana. »