Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Burundi, serikali kusaidia vituo vya habari vilivyoharibiwa wakati wa machafuko:Djinnit

Nchini Burundi, serikali kusaidia vituo vya habari vilivyoharibiwa wakati wa machafuko:Djinnit

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za maziwa makuu, Said Djinnit amesema serikali ya Burundi itasaidia kurejesha tena huduma za radio na televisheni zilizoharibiwa wakati wa maaandamano mapema mwezi huu kufuatia ghasia za kisiasa nchini humo.

Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Bujumbura Ijumaa baada ya mashauriano ya Alhamisi yaliyohusisha pande kadhaa pamoja na wasuluhishi kutoka Muungano wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mkutano wa kimataifa wa maziwa makuu, ICGLR.

Akinukuu kauli ya Djinnit, msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kufuatilia uchaguzi nchini Burundi, MENUB,Vladmir Monterio amesema baadhi ya wafuasi wa vyama vyenye misimamo mikali walisusia lakini matokeo nikwamba.. ..

(Sauti ya Vladmir)

“Serikali zitasaidia suala la ufunguaji wa redio na televisheni zilizofungwa na kuharibiwa wakati wa jaribio la mapinduzi ya kijeshi. Hiyo ni hatua moja na pia hatua nyingine mpya kwa upande wa radio kufanya kazi pamoja kwa kutumia studio ya Idara ya habari na kumaliza suala la ubinyaji wa habari na kuwapatia chanzo kingine cha habari”.

Kwa mujibu wa Djinnit mashauriano ya kisiasa nchini Burundi yataendelea baada ya mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kitakachofanyika Jumapili jijini Dar es salaam nchini Tanzania.