Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za tumbaku, biashara na kilimo chake

Athari za tumbaku, biashara na kilimo chake

Tarehe 31 mwezi Mei ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku, Shirika la Afya Duniani WHO likieleza kwenye ujumbe wake wa siku hiyo kuwa,  tumbaku huua watu milioni 6 kila mwaka duniani kote.Pamoja na kuendelea kupigia chepuo umuhimu wa kudhibiti matumizi ya tumbaku, WHO mwaka huu imesisitiza hatari za biashara haramu ya sigara ambayo ni changamoto ya afya, uchumi na usalama kwa baadhi ya nchi.

Miongoni mwa vifo milioni 6 vinavyotokea kila mwaka, 600,000 havisababishwi moja kwa moja na uvutaji wa sigara, lakini na kukaa karibu na wavutaji au kushiriki kwenye kilimo cha tumbaku. WHO imesisitiza kuwa watoto wanaolima tumbaku wako hatarini zaidi kuambukizwa ugonjwa kupitia mikono yao inapogusa majani ya tumbaku.

Uganda ni mojawapo ya nchi ambako, mbali na kuleta faida kwa uchumi wa nchi, kilimo cha tumbaku kinaathiri afya ya wakulima na maendeleo ya jamii. Kulikoni ? Ungana na John Kibego kwenye makala hii.