Tunaangalia ushirikiano wetu na FIFA:UM

29 Mei 2015

Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa makini ubia wake na shirikisho la soka duniani FIFA kufautia tuhuma za rushwa zinazowakabili maafisa wa ngazi za juu katika shirikisho hilo.

Akijibu swali katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu,  Stephanie Dujarric amesema wamekuwa na ushirikiano na FIFA kwa muda mrefu katika kombe la dunia na mambo mengine ya kimichezo na kuongeza kuwa hata hivyo mamlaka zinaoendesha uchunguzi dhidi ya tuhuma za zinazowakabili maafisa wa FIFA hazijawahusisha hadi sasa.

Bwana Dujarric amefafanua kuwa Umoja huo umekuwa uikitumia michezo kusambaza ujumbe wa maendeleo, stahamala  na nguvu ya mabadiliko na kuongeza kuwa ushirikiano huo umehusisha pia mashirikisho mengine ya michezo katika ngazi ya kimataifa na kitaifa.

Hata hivyo amesema ni mapema sana kuzungumza lolote wakati huu uchunguzi ukiendelea.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud