Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya wakimbizi waliokuwa Burundi warejea makwao: UNHCR

Mamia ya wakimbizi waliokuwa Burundi warejea makwao: UNHCR

Mwezi mmoja baada ya machafuko ya kisiasa nchini Burundi kulikosababisha kuzorota kwa ustawi wa kijamii na kiucumi husuani katika jiji la Bujumbura, wakimbizi waliokuwa wamejihifadhi nchini humo wameliomba shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR kuwarejeseha makwao huku wengine wakitaka kupelekwa sehemu zenye usalama zaidi.

Katika mahojinao na Joseph Msami kutoka Burundi, Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini humo Abel Mbilinyi amesema licha ya kupungua kwa wale wanaokimbilia nchi jirani wakimbizi waliokuwa Burundi kwa muda mrefu wametatizwa na hali ya usalama.  Awali anaanza kuelezea habari njema za kupungua kwa  wakimbizi wanaovuka mipaka.

(SAUTI MAHOJIANO)