#PKDAy: Sasa wanawake wanahitajika zaidi kwenye ulinzi wa amani: Edith

#PKDAy: Sasa wanawake wanahitajika zaidi kwenye ulinzi wa amani: Edith

Ikiwa leo ni siku ya walinda amani duniani, Umoja wa mataifa unaendelea kupigia chepuo harakati za kuimarisha uwezo wa vikosi vyake kwa kuwapatia vifaa vya kisasa na watendaji wenye stadi za kutosha kuweza kuhimili changamoto ziibukazo kwenye medani. Sanjari na hilo ni kuimarisha uwepo wa wanawake wakati huu ambapo wanawake kwenye mizozo hukabiliwa na shida nyingi ambazo penginepo zinaweza kukabiliwa vizuri na wanawake wenzao. Katika mahojiano kwa njia ya simu kutoka Darfur na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, mmoja wa walinda kutoka Tanzania, Edith Martin Swebe ambaye ni mshauri wa Polisi kwenye Ujumbe wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID huko Darfur Sudan, anatathmini siku hii adhimu, kile walichofanya ,akianza kwa kueleza ameipokea vipi siku hii.