Rwanda yatuzwa kuhusu teknohama huko WSIS

Rwanda yatuzwa kuhusu teknohama huko WSIS

Wakati  jukwaa la dunia kuhusu jamii na mawasiliano ulimwenguni, WSIS, linamaliza kikao chake leo mjini Geneva, tume ya kitaifa ya Rwanda ya vyombo vya Habari imeshinda tuzo kuhusu jamii na teknolojia ya habari na mawasiliano, TEKNOHAMA.

Tuzo hiyo iimetolewa kwa mashirika au mamlaka 18 duniani kote ambazo zinajitahidi zaidi katika kujenga jamii jumuishi kupitia TEKNOHAMA.

Akizungumza na idhaa hii, Julius Ndayisaba, Katibu Mtendaji wa Tume ya kitaifa ya Rwanda, amesema tume hiyo imetambuliwa kwa juhudi zake katika kudhibiti maadili ya vyombo vyote vya habari nchini Rwanda, siyo tu gazeti na redio, lakini pia Intaneti, na hivyo kuwezesha Wanayarwanda wengi zaidi kupata ujuzi na habari kupitia mtandao huo bila kukiuka maadili.

Ameongeza kwamba waandishi wa habari wengi wanatekeleza uhalifu mbalimbali kupitia mtandao wa Intaneti, wakidhani hawatafuatiliwa, ikiwemo kusambaza picha za ngono.

(Sauti ya Ndayisaba)