Harakati za UNICEF kuwasaidia wasichana kukabiliana na changamoto za hedhi Tanzania

28 Mei 2015

Nchini Tanzania Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF katika harakati za kukabiliana na usafi wakati wa hedhi, mwaka 2009 lilifanya utafiti ambao ulionyesha kwamba asilimia 11 ya shule 2,697 binafsi na za umma katika wilaya 16 ndio zenye vyoo vinavyokidhi angalau vigezo vya kuwezesha kujisafi ilhali  asilimia 9 vilkzingatia usafi huku asilimia moja tu vikiwa na sabuni.

Kadhalika huduma ya maji ilikuwa haipo katika baadhi ya shule ama imesambaratika. Kwa mantiki hiyo mradi wa maji, afya na usafi wa mazingira , WASH ulianzishwa ili kukabiliana na changamoto hizo. Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii John Mfungo ambaye ni mtaalam wa WASH katika UNICEF, Tanzania ameelezea kwa kina harakati hizo na hapa anaanza kwa kuelezea maana ya WASH

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter