Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari na nchi kuenziwa katika siku ya kimataifa ya walinda amani wa UM: Brigedia Jen Mohammed

Askari na nchi kuenziwa katika siku ya kimataifa ya walinda amani wa UM: Brigedia Jen Mohammed

Kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa hapo kesho Katibu mkuu Ban Ki-moon katika ujumbe wake pamoja na mambo mengine ametaka nchi wanachama kutoa ushirikiano wa kifedha na askari  katika  vikosi vya kulinda amani akisisitiza kuwa operesheni za kulinda amani lazima zifanyike kisasa na kiteknolojia zaidi.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Ofisi ya Kijeshi ya Idara ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa, DPKO, Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed amesema kuelekea  siku hii adhimu maandalizi yanaendelea ambapo pamoja na mambo mengine ametaja mambo yatakayofanyika ikiwa nisehemu ya kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha na wale wanaoendelea na zoezi hilo.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii mjini New York Brigedia Jenerali Mohammed anasema hafla tatu muhimu zitafanyika ikiwamo kuweka shada la maua ili kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha pamoja na

(SAUTI BRIGEDIA MUHAMMED)