Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF Tanzania yachukua hatua kuhakikisha hedhi haikwamishi wasichana shuleni

UNICEF Tanzania yachukua hatua kuhakikisha hedhi haikwamishi wasichana shuleni

Suala la hedhi kwa wasichana limesalia jambo la siri katika jamii barani Afrika ikiwemo nchini Tanzania ambapo wasichana wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi wakati wa siku zao, hiyo ni kauli ya John Mfungo ambaye ni mtaalam wa maji, afya na usafi wa mazingira WASH katika Shirika la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania alipohojiwa na Idhaa hii.

Amesema kwa mantiki hiyo UNICEF imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kutoa muongozo wa ujenzi wa vyoo , kuelimisha walimu na  wasichana wenyewe ili kukabialiana na changamamoto zilizopo ikiwemo…..

(Sauti ya John)

Bwana Mfungo amesema kwamba ushiriki wa serikali na wadau ni muhimu katika kuhakikisha kwamba mazingira bora kwaa wasichana wakati wa hedhi yanafikiwa ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye masomo yao..