Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mizozo maeneo mbali mbali Afrika yaongeza shinikizo la kibinadamu Sahel:Piper

Mizozo maeneo mbali mbali Afrika yaongeza shinikizo la kibinadamu Sahel:Piper

Idadi ya watu wanaokimbia makazi yao kutokana na mizozo inayoendelea kwenye nchi zilizoko ukanda wa Sahel barani Afrika imeongezeka kutoka Milioni Moja nukta Nne hadi Milioni Tatu nukta Sita katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Grace)

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda wa Sahel, Robert Piper alizotoa alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi baada ya kuwapatia muhtasari wa hali halisi wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja huo.

Amesema mizozo na majanga huko Kaskazini-mashariki mwa Nigeria, Mali, Darfur-Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati inaongeza shinikizo la kibinadamu Sahel na kuleta changamoto kama vile Mosi ukimbizi wa ndani na pili ..

Tunashughulika na ongezeko la mazingira magumu zaidi ya kufanya kazi ikiwemo kufikia wahitaji, ukosefu wa usalama na vitisho kwa wafanyakazi wetu na wadau wetu. Na tatu ni matatizo ya ulinzi.”

Ametoa wito kwa nchi wanachama kutosahau eneo hilo akikumbusha kuwa hadi sasa katika ombi la mwaka huu la dola bilioni Mbili wamepata asilimia 20 tu.