Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano kuhusu usalama wa kompyuta na nyuklia kufanyika IAEA

Kongamano kuhusu usalama wa kompyuta na nyuklia kufanyika IAEA

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA, limeandaa  kongamano kuhusu usalama wa kompyuta katika mazingira ya ulimwengu wa nishati ya nyuklia, ambalo litafanyika kwenye makao yake makuu mjini Vienna, Austria.

Kongamano hilo la Juni 1 hadi 5, litawaleta pamoja wawakilishi wa mamlaka za nyuklia na wasimamizi wa mitambo ya nyuklia, watekelezaji wa sheria, pamoja na mashirika ya kikanda na kimataifa.Kongamano hilo ndilo la kwanza kabisa kufanyika kuhusu suala la usalama wa kompyuta kwenye mitamabo ya nyuklia.

Kongamano linaandaliwa kwa ushirikiano na shirika la polisi ya kimataifa, INTERPOL, Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU, Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Utafiti baina ya kanda kuhusu uhalifu na haki, UNICRI, na Kamisheni ya Kimataifa ya Taaluma ya Elektroini, IEC, na litawaleta pamoja zaidi ya wataalam 650 kutoka nchi 17 na wawakilishi wa kikanda na kimataifa