Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kurudi nyumbani kwa Wasomali walioko Yemen

Ni wakati wa kurudi nyumbani kwa Wasomali walioko Yemen

Shirika la uhamiaji duniani IOM linasaidia watu wanaokimbia mzoo unaoendelea nchini Yemen wakiwemo raia wa Somalia

Kulingana na takwimu za IOM watu zaidi ya elfu tisa wamewasili Somalia wakikimbia mapigano nchini Yemen.

Wakati mzozo wa Yemen, maelfu ya wanawake, watoto na wanaume wakiwemo wakimbizi 250,000 wa Somalia sambamba na wahamiaji bado wamekwama nchini Yemen.

Kwa kushirikiana na wadau, IOM imekuwa ikiwasaidia raia hao wa Somalia kurejea nyumbani. Basi ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo