Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban anakshi ujumbe kwenye daraja la Tomorrowland huko Ubelgiji

Ban anakshi ujumbe kwenye daraja la Tomorrowland huko Ubelgiji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye sasa yuko ziarani Ubelgiji amepatiwa heshima ya kunakshiwa ujumbe wake kwenye daraja maalum linalojengwa kuelekea eneo ambako hufanyika tamasha kubwa la muziki kila mwaka la Tommorowland.

Ban kwenye ujumbe wake wa daraja hilo lijulikanalo kama dunia moja, ameandika maneno Hebu tufanye kazi pamoja kufikia utu kwa wote ambapo amesema itakuwa ni fursa kwa wapitao kujikumbusha umuhimu wa amani.

Katibu Mkuu ameshukuru waandaaji wa tamasha hilo linalofanyika Julai kwa kumwalika na kunakshi ujumbe huo kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.

Amesema ni matumaini yake kuwa daraja hilo pamoja na tamasha hilo linalokutanisha vijana na wanamuziki zaidi ya Laki Mbili litatoa fursa kwa washiriki kutumia muziki na kuonyesha ubunifu wao wa jinsi ya kufanya dunia iwe pahala salama na kujenga ustawi kwa maendeleo endelevu.